Jibu Kwa Ajili Yako
Je, wajua kwamba kuna mtu ambaye hujua yote juu yako? Ni Mungu aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo. Yesu, Mwana wa Mungu, pia hujua yote ambayo umeshafanya. Yeye hujua yaliyopita, ya leo, na yajayo. Yeye anakupenda na alikuja ulimwenguni kukuokoa kutoka dhambini. Anao mpango wa uzima wako ili kukuletea furaha.
Siku moja Yesu alikuwa akitembea na rafiki zake alienda katika kijiji cha Samaria. Yesu alikaa kando ya kisima wakati rafiki zake walienda kununua chakula.
Yesu alipokuwa amekaa pale, mwanamke mmoja alikuja kuchota maji kisimani. Yesu alimwambia, “Naomba unipe maji ninywe.”
Maandiko kamili ya: Jibu Kwa Ajili Yako
Mwanamke alishangaa, akasema, “Je, unaniomba maji unywe? Je, kwani hujui mimi ni Msamaria, na ninyi Wayahudi hamna uhusiano nasi?”
Kwa upole Yesu alijibu, “Kama kwa hakika ungemjua Mungu, na ni nani anayeongea nawe, ungeniomba Mimi nikupe maji ya uzima, na ningeshafanya kwa furaha.”
Mwanamke huyo alimtazama kwa mshangao, akasema, “Bwana, kisima ni kirefu, Je, utachotaje maji ya uzima na huna chombo?”
Yesu akajibu tena, “Wale wanaokunywa maji ya kisima hiki, watapata kiu tena, lakini ukinywa maji ninayoweza kutoa, kamwe hutapata kiu tena.”
Mwanamke huyo alisema, “Bwana, nipe maji hayo ili nisipate kiu tena, wala nisihitaji kurudi kuchota maji hapa.”
Yesu alimwambia, “Nenda umwambie mume wako na uje naye hapa.”
Alijibu, “Sina mume.”
Yesu alisema, “Ni kweli. Umeshakuwa na wanamume watano, lakini mmoja unaye sasa siye mume wako”.
Yule dada alijiuliza akistaajabu, Mtu huyu anajuaje habari zangu? “Bwana, ninaweza kuona kwamba wewe ni nabii. Watu wangu walimwabudu Mungu mahali hapa hapa, ninyi mnasema kwamba Yerusalemu ndiyo mahali ya ibada.”
Yesu alimwambia, “Hakuna mahali muhimu twaweza kumwabudu, waumini wa kweli leo wanaweza kumwabudu Baba katika Roho na kweli popote.”
Mwanamke yule alisema, “Najua kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja, na atakapokuja, atatuelezea yote.”
Kisha Yesu alimwambia kwa uwazi, “Ndiye Mimi.”
Basi yule dada aliacha mtungi wake wa maji akarudi mjini. Aliita, “Njooni! Njooni na kumwona mtu ambaye ameniambia mambo yote niliyowahi kutenda. Je, yeye siye Kristo?”
Kisha watu wakatoka mjini kumlaki Yesu. Wengi waliamini kwamba yeye ndiye Kristo Mwokozi, kwa sababu alijua habari zao zote. Unaweza kusoma habari hii katika Biblia, katika Injili ya Mtakatifu Yohana 4:3-42.
Yesu hujua habari zetu zote, mema pamoja na mabaya. Tungependa kuficha mabaya ambayo tumetenda katika maisha yetu, lakini hatuwezi kumficha Yesu. Amekuja kutuokoa kutoka kwenye adhabu tunayostahili kwa kufanya uovu. Anaweza kuondoa mzigo mzito ule unaohisi katika moyo wako, na kukupa amani. Alikufa ili aondoe dhambi zako na kwamba akufanyie uwezekano wa kwenda mbinguni utakapofariki.
Yesu ndiye jibu la maswali yako yote, na mahitaji yako yote. Yeye anataka awe rafiki yako. Anatamani ajaze moyo ulio tupu. Anaweza kubadilisha wasiwasi na hofu yako kwa amani na utulivu.
Yesu husema, “Njooni Kwangu….. na nitawapumzisha.” (Mathayo 11:28) Mwombe tu Mungu, na mwambie una huzuni kwa ajili ya dhambi zako. Mwombe Yesu aje katika maisha yako. Unapomkabidhi Mungu Mkuu huyu binafsi yako kwa imani, atakaa moyoni mwako. Na uwepo wake utakupa shangwe. Atakufanya uwe na lengo lenye maana, uwe na makusudi, na uwe na nguvu katika maisha yako. Atakuwa jibu kwa ajili yako.